Rules & Regulations


 • Kusimama na kumsalimia mtu yoyote anayemzidi umri anapoitwa,anapoingia darasani au kwenye mkusanyiko/mkutano.
 • Kutumia Lugha nzuri wakati wote kati yao wenyewe, kwa walimu na watu wengine.
 • Kuheshimu Bendera ya Taifa, picha za viongozi wa Serikali nembo ya Taifa "Coat of Arms" na wimbo wa Taifa.
 • Kuheshimu ofisi za Shule, mali binafsi na mali ya umma.
 • Kutovuta siagara kufunga ndevu au kucha na kuwa na nywele zisizowekwa katika hali ya usafi.
 • Kuvaa sare inayojulikana kwa wanafunzi na jumuiya nzima na iwe katika mshono unao kubalika na kulingana na heshima inayosisitizwa kitaifa.
 • Kuwepo ndani ya eneo la shule (sehemu) husika kwa muda wote wa masomo.
 • Kufika shuleni siku zisizokuwa za masomo kwa kibali au ruhusa maalum.
 • Mwanafunzi haruhusiwi kuchangia mchango wowote ule bila ya kibali.
 • Mwanafunzi haruhusiwi kuruka uzio/ukuta wa shule.
 • Mwanafunzi haruhusiwi kuwa nyuma ya jengo jipya ( Bakhresa) kwa muda wowote ule.
 • Hairuhusiwi wanafunzi kuwepo eneo la shule baada ya masomo kwisha yaani saa 12.00 jioni isipokuwa kwa shughuli maalum iliyopata kibali cha Uongozi wa Shule.
 • Mwanafunzi anapaswa atoe taarifa kwa tukio lolote la uhalifu kwa Uongozi wa Shule/walimu wa zamu.
 • Mwanafunzi anapaswa kufanya mitihani yote bila kukosa isipokuwa kwa taarifa maalum.
 • Mwanafunzi anapaswa kuhudhuria masomo rekebishi "remedia classes" yanayotolewa shuleni "remedial classes" muda wowote baada ya masomo siku za kawaida au wakati wa likizo.
 • Mwanafunzi anapaswa kuwahi shule au sehemu yeyote atakapohitajika mfano kwenye sherehe za muungano n.k.
 • Mwanafunzi anapaswa kuyapenda masomo yote anayofundishwa/kusoma mchepuo wake mfano kidato cha I na II masomo yote wanapaswa wayapende na kuyasoma kwa bidii. Kidato cha V na VI masomo ya ziada General Studies na BAM yanapaswa kusomwa sawa na masomo ya Combinations mfano HKL, PCM, PCB n.k
 • Mwanafunzi atawajibika kufanya usafi na kutunza mazingira na mali za shule sehemu zote atakazopangiwa.
 • Kufika kwa haraka eneo husika wakati wa kengele ya dharura.
 • Mwanafunzi anapaswa kuhudhuria vipindi vya dini bila kukosa na kwa wakati.
 • Mwanafunzi haruhusiwi kugombana na mwanafunzi mwenzake, mwalimu au mtu yoyote yule
 • .
 • Mwanafunzi haruhusiwi kuandika maandishi pasipotakiwa mfano ukutani, vitabuni n.k.
 • Mwanafunzi haruhusiwi kutumia simu katika maeneo ya shule (yaani ndani na nje ya darasa) isipokuwa kwa kibali kutoka kwa uongozi wa shule.
 • Mwanafunzi haruhusiwi kuhubiri dini awapo shuleni isipokuwa kwenye kipindi cha dini.
 • Mwanafunzi anapaswa kukubali uteuzi wowote ule mfano kushiriki katika michezo, maandamano yaliyorasmi n.k.
 • Mwanafunzi haruhusiwi kutoa/kubandika tangazo bila kibali.
 • Mwanafunzi haruhusiwi kufanya biashara shuleni.
 • Mwanafunzi hapaswi kwenda kwenye maeneo ya baa kumbi za starehe akiwa na sare za shule/nguo za nyumbani.
 • Mwanafunzi haruhusiwi kuja na silaha shuleni.
 • Mwanafunzi wa kike kidato cha I - IV haruhusiwi kusuka nywele.